Rapper maarufu nchini Marekani, Nicki Minaj ametishia kumpeleka mahakamani mtangazaji, Jesse Palmer wa kituo cha DailyMailTv baada ya kutoa taarifa za mpenzi mpya wa Nicki Minaj.

Taarifa za mpenzi mpya wa Nicki Minaj kuhusishwa na matukio ya mauaji na ubakaji kitu ambacho kilipelekea kufungwa jela zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, huku mtangazaji Jesse Palmer akizungumza juu ya Kenny Petty kwenye kipindi cha luninga taarifa ambazo zimemchafua rapper Minaj ambapo ameapa kumpeleka mahakamani.

Aidha Nicki Minaj ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kwamba, “Ni vyema ukapata mwanasheria mzuri, Jesse Palmer. umezungumza uongo kuhusu mimi kwenye televisheni na sasa nakushtaki. ni vyema ukaweza kutetea ulichokisema kuhusu mimi tena kwa ushahidi.”

Serikali yazipatia mabilioni ya fedha kampuni za mawasiliano
Polisi wanawake wapongezwa jijini Arusha

Comments

comments