Mwanamziki wa Bongo fleva, Rich Mavoko amewachanganya mashabiki wake mara baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagramu ujumbe ambao umeacha maswali mengi huku wengi wakijiuliza dhumuni la msanii huyo kuandika hivyo lilikuwa ni lipi.

Katika ukurasa wake wa Instagram Mavoko ameandika kuwa ni siku yake ya mwisho ya maisha yake yaliyobaki, ujumbe ambao umeacha maswali mengi kwa mashabiki wake.

”Ni siku yangu ya mwisho ya maisha yangu yaliobaki ”Ameandika Rich Mavoko

Aidha, mashabiki wa msanii huyo wengi wanahisi labda anataka kujiua kulingana na mziki wa bongo fleva kuwa mgumu huku wengi wakidai kuwa ni msongo wa mawazo,

Hata hivyo, Wezele ndio wimbo wa mwisho kuachiwa na msanii huyo Desemba 12, 2018 kupitia mtandao wa youtube, huku taarifa za watu wa karibu wa Rich Mavoko wakisema kuwa yupo mbioni kutoa wimbo mpya amabo utakuwa ni Insparation song.

Meya wa Manispaa ya Lindi awaonya Wafugaji
Malawi: Joyce Banda ajiengua mbio za urais

Comments

comments