Shirikisho la soka barani Ulaya, limetoa orodha ya mwisho ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2015 barani humo.

Orodha ya mwisho iliyotolewa na UEFA imewajumuisha washambuliaji wawili wa FC Barcelona Lionel Messi na Luis Suarez ambao watapambana na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.

Ronaldo alifanikiwa kushinda tuzo hiyo mwaka 2014 huku mpinzani wake wa karibu Lionel Messi aliwahi kuwa mshindi mwaka 2011 akifuatiwa na Andres Iniesta mwaka 2012 na kisha Franck Ribery mwaka 2013.

Waandishi wa habari kutoka nchi wanachama wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, watakutana na kuwapigia kura watatu hao na kisha matokeo yatatangazwa kwenye hafla maalum itakayofanyika August 27 mjini Monaco nchini Ufaransa.

Siku hiyo UEFA watapanga makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa ajili ya msimu wa 2015-16.

Kabla ya wachezaji hao watatu kutajwa usiku wa kuamkia hii leo na kuingia kwenye hatua ya mwisho, UEFA ilikuwa na orodha ya wachezaji kumi ambao walikua wakiwania tuzo ya mchezaji bora wa barani Ulaya mwaka 2015.

Katika ligi ya nchini Englnd kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ublegiji na klabu ya Chelsea Eden Hazard (10) alikua pekee katika orodha hiyo sambamba na wachezaji kutoka kwenye klabu ya Juventus  Gianluigi Buffon (4), Andrea Pirlo (7), Arturo Vidal (8), Carlos Tevez (9), Paul Pogba (10) pamoja na mshambuliaji wa FC Barcelona  Neymar aliyeshika nafasi ya (5).

Muhimu: namba zilizopo kwenye mabano ni nafasi ya mchezaji katika ushindani wa tuzo ya barani Ulaya mwaka 2015.

Ali Kiba Kufanya Collabo Na Ne-Yo
Azam FC Yashinda Mchezo Wa 10 Mfululizo