Kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kimeendeleza moto wa kufanya vyema katika michezo ya kujiandaa na mshike mshike wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana, kwa kuichapa timu ya vijana ya Msumbiji.

Mchezo huo uliounguruma kwenye uwanja wa  taifa jijini Dar es salaam, ulishuhudia vijana hao wanaonolewa na kocha Ammy Ninje wakiendeleza wimbi la ushindi kupitia kwa Abdul Suleiman pamoja na winga wa klabu ya Youngh Africans, Said Mussa Bakari ‘Side Ronaldo’ aliyepika bao la kwanza lililokuwa la kusawazisha kipindi cha kwanza, kabla ya kufunga bao la pili kipindi cha pili.

Msumbiji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 13 kwa penati mfungaji Belarmino Manhce, kufuatia kipa wa Tanzania kumchezea rafu Martinho Alberto na refa Emmanuel Mwandembwa wa Morogoro kuamuru mkwaju huo.

Katika mchezo wa kwanza wa kujipima nguvu uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, Ngorongoro Heroes waliifunga timu ya vijana ya Morocco bao moja kwa sifuri, lililowekwa wavuni na Abdul Suleiman.

Ngorongoro Heroes watapambana na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo katika mchezo wa hatua ya kwanza wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, mwezi ujao.

Magazeti ya nje na ndani ya Tanzania leo Machi 22, 2018
Welayta Dicha kuamua safari ya Young Africans