Nyota wa Brazil, Neymar da Silva Santos Júnior, amesema hana budi kujipa matumaini ya kupona kwa wakati, ili kufanikisha lengo la kuisaidia timu yake ya taifa katika fainali za kombe la dunia nchini Urusi.

Mshambuliaji huyo wa klabu bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain amelazmika kuweka wazi mustakabali huo, baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, jambo ambalo lilikua linaziusha hofu miongoni mwa mashabiki wake.

Neymar alikuwa kimya tangu alipopata majeraha ya mguu wakati wa mchezo wa ligi ya Ufaransa dhidi ya Olympic Marseille mwezi Februari, lakini kurejea kwake katika mazoezi mepesi kumempa faraja na kuamini huenda akawa sehemu ya kikosi cha Brazil kitakachokwenda Urusi kuusaka ubingwa wa dunia.

“Naamini muda uliosalia unatosha kuniwezesha kuwa sehemu ya kiksoi cha Brazil, hakuna linaloshindikana zaidi ya kufuata utaratibu wa mazoezi ninayopangiwa kuyafanya kila siku,” Amesema Neymar

“Kila kitu kinakwenda vizuri mpaka sasa, hata madaktari wanaofuatilia maendeleo yangu wananipa matumaini ya kuwa sehemu ya timu ya taifa.

“Ninahitaji sana kuichezea timu yangu ya taifa katika fainali za mwaka huu, ikitokea ninashindwa kuwa sehemu ya timu itakayokwenda Urusi nitahuzunika, lakini nina uhakika nitakua mmoja wa wachezaji watakaokua fit kwa fainali hizo.”

Neymar ambaye ni nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil, alikuwa miongoni mwa wachezaji walioshindwa kufanya vyema kwenye fainali za 2014 zilizofanyika nchini kwao, na kuambulia kisago cha aibu kutoka kwa Ujerumani cha kufungwa mabao saba kwa moja, katika hatua ya nusu fainali.

Katika fainali za mwaka huu, Brazil imepangwa katika kundi E, na itaanza kuusaka ubingwa wa dunia kwa kucheza dhidi ya Uswiz mjini Rostov, Juni 17.

Mataifa mengine yaliopangwa katika kundi hilo ni Costa Rica ambao watacheza dhidi ya Brazil Juni 22 mjini Saint Petersburg, na Sebia ambao watacheza dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria duniani Juni 27 mjini Moscow.

Sam Allardyce ambwatukia bosi wa DC United
Bwawa lililobomoka na kuua makumi Kenya lilijengwa 'kihuni'