Meneja mpya wa klabu ya Newcastle Utd, Steve McClaren ametangaza mipango ya kufanya vyema msimu ujao wa ligi kwa kusema anahitaji kukiongezea nguvu kikosi chake.

McClaren amesema anahitaji kufanya usajili wa wachezaji watano katika nafasi tofauti ili kutimiza mikakati ya maandalizi ambayo yameanza mwezi huu kwa kuamini hakuna kitakacho shindikana.

Meneja huyo aliyechukua nafasi ya John Caver aliyekua meneja wa muda klabuni hapo, amesema tayari ameshafanya mazungumzo na mmiliki wa klabu ya Newcastle Utd, Mike Ashley pamoja na kuwasilisha mapendekezo ya wachezaji anaowahitaji kabla ya kuingia vitani kuanzia mwanzoni mwa mwezi ujao.

Hata hivyo, pamoja na kuzungumza na vyombo vya habari bila kuwataja wachezaji aliowapendekeaza ili wasajiliwe kikosini mwake, tayari imeanza kuhisiwa huenda kiungo wa klabu ya PSV Eindhoven, Georginio Wijnaldum pamoja na mshambuliaji wa klabu ya QPR Charlie Austin ni sehemu ya wanaotarajiwa huko St James Park.

McClaren alichukua kijiti cha kuwa mkuu wa benchi la ufundi klabuni hapo baada ya kupata madhila ya kutimuliwa kwenye klabu ya Derby County inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza.

Nape Ayabariki Majina Matano Yaliyopitishwa, Magufuli Asema 'Neno'
Urais CCM: Majina Matano Haya Hapa, Dr. Nchimbi Apinga Uamuzi