Wizara ya kilimo imegawa vifaa vya kielektroniki  katika vyuo 14  vya kilimo   nchini vyenye thamani ya Tsh.Milioni 248.69 ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vitabu vya kujifunzia katika vyuo vya kilimo hapa nchini,.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma katika hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo vya TEHAMA , Katibu mkuu Wizara ya Kilimo  Gerald Msabila Kusaya  amebainisha kuwa  tangu ateuliwe tarehe 5,Machi mwaka huu, amefanya ziara katika vyuo mbalimbali vya elimu ya kilimo  hapa nchini na kubaini changamoto ya uhaba wa vitabu hivyo na kuamua kununua vifaa vya kielekroniki kwa ajili ya kujifunzia .


“Baada ya kuona changamoto hiyo tulijadili na wadau tukaona namna nzuri ya kusoma  kwa njia ya kielekrtoniki  hivyo tumeamua kununua kununua vifaa mbalimbali hali itakayosaidia wanafunzi wetu ambao ni wataalam wa baadae wa kilimo kujifunza kwa njia ya mtandao na vifaa hivyo vikigharimu Tsh.Milioni 248.69″ amesema Kusaya.

Kusaya ametoa wito kwa wakuu wa vyuo vya kilimo kuhakikisha wanasimamia vifaa hivyo vitumike vizuri na mara kwa mara ili kuwandaa  wataalamu wa kilimo wanaoendana na wakati.

Baada ya kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya Wakuu wa vyuo 14 vya serikali,mkuu wa chuo cha Kilimo Mlingani Samson Cheyo pamoja na kaimu mkuu wa chuo cha Sukari (NSI) kilichopo Kilombero koani Morogoro  Aloyce Kasmir wamesema vifaa hivyo vya TEHAMA vitarahisisha katika kujifunza.

Baadhi ya vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa ni pamoja na Rooter Machine, Kompyuta mpakato(laptop),Desk top pamoja na TV vikiwa na thamani ya shilingi milioni 248.6

Vandenbroeck: Yanga imefanya usajili mzuri
Magufuli aanza rasmi Kampeni