Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi kuhusiana na madai ya ubalozi wa Marekani nchini iliyoyatoa katika taarifa yake hapo jana kuhusu uchaguzi mdogo wa Agosti 12 kwenye jimbo la Buyungu na kata 36 nchini.

Taarifa iliyotolewa na NEC, kupitia  Ofisa Habari Mwandamiz, Christina Njovu tume imeutaka ubalozi huo uthibitishe inachokieleza juu ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu na kwenye kata 36 ikisema uchaguzi mdogo huwa hauna waangalizi wa kimataifa na kuhoji ubalozi wa Marekani umetoa wapi taarifa hizo na hayo ulioyaona ni kwa kutumia utaratibu upi na sheria ipi.

“Katika Jimbo la Buyungu mgombea wa ubunge wa Chadema, Elia Kanjaro aliongea na vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii akaeleza hisia zake na kusema bayana kuwa amekubaliana na matokeo na ameshukuru kwa kuwa uchaguzi huo umemjenga,”imesema taarifa hiyo

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa kilichotokea Arusha ni vurugu mitaani mbali na maeneo ya vituo vya kupigia kura, kwa kuwa vurugu hizo zilipelekea jinai kufanyika vyombo husika vinashughulikia.

Hata hivyo, hatua hiyo imekuja kufuatia taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini kuhusu uchaguzi wa marudio katika Kata 77 na jimbo la Buyungu uliofanyika mnamo Agosti 12, 2018 ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka katika ofisi za ubalozi huo imeeleza kuwa uchaguzi huo uligubikwa na matukio ya fujo na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi

 

 

RC Brigedia Jenerali Nicodemas amgomea mkandarasi
Victor Moses aibwaga Super Eagles