Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo Agosti 21, 2017 imeteuwa Madiwani wanawake wa viti maalum ili kujaza nafasi wazi za Madiwani katika Halmashauri mbalimbali Tanzania Bara.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa NEC, Kailima Ramadhani imeeleza kuwa Madiwani hao wameteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292,.

Amesema kuwa NEC imefanya kikao chake cha kawaida leo Agosti 21, 2017 na baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kumi na wawili (12)

Madiwani hao walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

NA. JINA CHAMA HALMASHAURI
  1. 1
Ndugu Saida Idrisa Kiliula CUF Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
Ndugu Sophia Charokiwa Msangi CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Ndugu Shahara Selemani Nduvaruva CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali
Ndugu Neema K. Nyangalilo CCM Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Ndugu Farida Zaharani Mohamed CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero
Ndugu Lucia Silanda Kadimu CCM Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui)
Ndugu Amina Ramshi Mbaira CCM Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu
Ndugu Janeth John Kaaya CHADEMA Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Ndugu Sara Abdallah Katanga CHADEMA Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Ndugu Ikunda Massawe CHADEMA Halmashauri ya Wilaya ya Hai
Ndugu Tumaini Wilson Masaki CHADEMA Halmashauri ya Wilaya ya Siha
Ndugu Elizaberth Andrea Bayyo CHADEMA Halmashauri ya Mji wa Mbulu

Aidha, ameeleza kuwa uteuzi huo umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hizo wazi.

 

Video: Makonda kusaidia watu 1000 miguu ya bandia
Video: Rais Shein alivyowafunda wanafunzi kuhusu yanayowazidi umri