Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameeleza jinsi CAG mpya Charles Kichere anavyotegemewa kufanya kazi na Bunge hilo.

Ameyasema hayo katika hafla ya kuapishwa kwa CAG huyo iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es salaam, na kubainisha kuwa wanamtegemea sana kama jicho la Bunge katika kuangalia matumizi mbalimbali jinsi yanavyoenda na kutoa ushauri.

” Tunapitisha bajeti kama bunge kwa kila eneo la serikali na matumizi yake…serikali ikisha tumia wewe CAG ndiyo jicho letu unaenda kupitia na kukagua matumizi yote halafu unatuletea  zile taarifa bungeni” Amesema Ndugai

“Tunakutegemea sana kama jicho letu, jicho ndiyo kila kitu kwa mwanadamu, ukikosa jicho siyo rahisi kujua unaelekea wapi, wewe ni chombo muhimu sana.., Ni jicho la Taifa letu” amesisitiza Ndugai.

Amesema kuwa Bunge linamtegemea pia CAG kushauri namna matumizi mbalimbali yanavyoenda na jinsi ya kurekebisha kwa kushirikiana na kamati za LAAC na PAC.

Aidha amowapongeza wote walioteuliwa na Rais kushika nyadhifa mbalimbali kwani wamepata imani kutoka kwa Rais na watanzania wote kwani ndiyo waliomuamini Rais Magufuli.

Rais Magufuli ampa ujumbe mzito CAG mpya, "Usibishane, kasafishe uchafu..."
LIVE IKULU: Rais Magufuli akiapisha viongozi mbalimbali

Comments

comments