Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 176 imeanguka Iran na kupoteza maisha ya abiria na wahudumu wote waliokuwa wakisafiri ndani ya ndege hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na vyombo vya habari nchini humo.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran.

Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.

Ubalozi nchini humo umeripoti kuwa ajali hiyo imesababishwa na injini ya ndege hiyo kufeli na kusababisha kuanguka muda mchache tu mara baada ya kuanza kupaa katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini.

Aidha, haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani.

Hata hivyo kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege ilianguka.

Hii si mara ya kwanza tukio kama hilo kutokea nchini Iran, kwani mara kadhaa kumekuwa kukitokea majanga kama hayo ya ndege kulipuka na kusababisaha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha na baadhi ya mali.

Ambapo mnamo mwaka 2009 ndege ililipuka katika mji wa Qazvin na kuua watu 168 wakiwemo wahudumu waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Pia  mnamo mwaka 2011 ndege ya kiiran katika mji wa Orumiyeh ililipuka kutokana na hali mbaya ya hewa na kuuwa watu 77.

Huku mwaka 2018 ililipuka katika kijiji cha Kohangan kusini mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 65.

 

Dkt. Kigwangalla aliwashia moto gazeti la Jamhuri kwa kumchafua
Video: Vita mpya Chadema, Marekani, Iran zaiweka dunia njia panda