Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye hivi karibuni amekihama chama cha CCM na kujiunga na CHADEMA, ameshindwa kupanda jukwaani na kuhutubia mkoani Mtwara kama ambavyo iliarifiwa na uongozi wa CHADEMA.

Akithibitisha hilo mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa kukosekana kwa ndege inayofanya safari kati ya Dar es Salaam na Mtwara kumemsababishia Nyalandu kushindwa kuhudhuria mkutano huo, kwani alikuwa Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Tundu Lissu.

Amesema kuwa Nyalandu amefika Dar es Salaam na kukosa ndege ya kwenda Mtwara, hivyo amewaomba radhi wananchi ambao walikuwa wanasubiria kumsikiliza na kwamba wanaandaa kwa ajili ya siku nyingine kuweza kufanya hivyo.

“Tunaomba radhi kwa hili ila tukio hilo tunaliandalia mahali pengine na wakati ukifika tutakuwa pamoja naye,”amesema Mrema

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Jumamosi akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam alisema amempokea Nyalandu na Jumapili Novemba 12, 2017 angeungana naye kwenye mkutano wa kampeni mjini Mtwara

Majirani: Dk Shaka ‘Mnunuzi’ wa Majumba ya Lugumi ana roho ya kipekee
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 13, 2017