Rubani na abiria wamefariki katika ajali ya ndege ndogo ya Shirika la Auric Air, iliyoanguka katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti Arusha  Nchini Tanzania.

Ndege imepta ajali leo jumatatu asubuhi septemba 23, 2019 katika uwanja mdogo wa ndege ndani ya hifadhi ya taifa ya serengeti.

Ajali hiyo imetokea sa 1:30 asubuhi ambapo ilikuwa ikiruka kutoka Serengeti kwenda Arusha baada ya kushusha watalii, ambapo katika ajali hiyo Rubani na abiria mmoja wamefariki dunia.

Kamishna msaidizi mwandamizi wa shirika la hifadhi za taifa (TANAPA), Paschal Shelutete akizungumza na Mwananchi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

”Tunatoa tarifa zaidi baadae kwni sasa kazi inayoendelea ni kuokoa vitu na kuhifadhi miili” amesema kamanda Shelutete.

 

Diamond 'apagawisha' JAMAFEST
Solskjaer: Umaliziaji ni tatizo Manchester United