Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Ettiene Ndayiragije amesema kiungo wa Simba SC Jonas Mkude hakufanya kitendo cha utovu wa nidhamu kama ilivyokua inaripotiwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari.

Ettiene alimjuimuisha Mkude kwenye kikosi cha wachezaji 35 waliokuwa wanajiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Tunisia na michuano ya Mataifa Bingwa Barani Afrika (CHAN 2020), lakini kiungo huyo hakuripoti kambini, hadi ilipovunjwa kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Kocha huyo kutoka Burundi amesema kulikuwa hali ya kuchelewa kwa taarifa za Mkude ambazo zilipitia kwa Meneja wa timu ya Taifa ambaye alipaswa kumfikishia yeye kama kocha mkuu.

“Sio kama watu walivyoichukulia hapo mwanzo, Mkude hakuwa mtovu wa nidhamu ila taarifa zilichelewa kunifikia lakini kila kitu kinaenda sawa,” alisema Ndayiragije.

Awali Mkude alikanusha taarifa hizo na aliahidi kukutana uso kwa macho na kocha Ndayiregije, ili kuweka mambo sawa.

Uganda: Watoto 11 waambukizwa Corona, wote wa kwaya moja
Museveni afunga maduka Uganda, Kugawa chakula bure

Comments

comments