Viongozi wa nchi 44 barani Afrika wamesaini makubaliano ya kufungua mipaka yao na kufanya kuwa eneo huru la biashara.

Makubaliano hayo ambayo yaliyofanyika Kigali nchini Rwanda katika kikao hicho cha viongozi wa wakuu wa nchi unazifanya nchi hizo kuwa moja kati ya maeneo makubwa zaidi duniani kama maeneo huru ya biashara.

Ripoti zinaeleza kuwa makubaliano hayo yanayoweza kuanza kutekelezwa ndani ya miezi 6 yataleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi takribani bilioni 1.2 barani Afrika.

Hata hivyo, nchi kumi za bara hilo ikiwa ni pamoja na Nigeria yenye idadi kubwa ya watu, hazikuwa miongoni mwa zilizosaini mkataba huo.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, nchi hizo zitaondoa ‘mageti’ ya biashara kati yao ikiwa ni pamoja na baadhi ya tozo za kuvusha bidhaa mipakani ili kuruhusu bidhaa kuingia nchi moja na nyingine kwa uhuru.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki amesema kuwa hiyo ni hatua nzuri kwa bara hilo akiita kuwa ni “changamoto ya kuamini, changamoto ya uthubutu na hali ya kujiamini kimafanikio.”

Rais wa Sudan azidi kuinyima usingizi ICC akiwa Rwanda
Trump ajipanga kuiwekea vikwazo China