Vituo vya kupigia kura vya nchi wanachama 21 wa Umoja wa Ulaya vitafunguliwa leo Jumapili, kwa uchaguzi wa bunge la Ulaya, ikiwa ni pamoja na mataifa makubwa ya umoja huo ambayo ni Ujerumani, Ufaransa, Italia, Hispania na Poland.

Mataifa hayo matano pekee yanatoa takribani nusu ya wabunge wa Bunge la Ulaya ambao ni 348 kati ya jumla ya wabunge 751.

Aidha, upigaji kura wa bunge pekee la kimataifa duniani ulianza Alhamis nchini Uholanzi na Uingereza. Ireland na Jamhuri ya Czech zilipiga kura hiyo Ijumaa iliyopita na Latvia, Malta pamoja na Slovakia ambazo zilipiga kura jana Jumamosi.

Jumla ya wananchi milioni 420 wana haki ya kupiga kura, ambapo watafiti wamesema kuwa wanatarajia idadi ya wananchi watakaojitokeza kupiga kura itaongezeka kidogo ikilinganishwa na asilimia 43 tu ya mwaka 2014.

Dhahabu ya bilioni 34.3 yauzwa kwa kipindi cha mwezi mmoja
Tuhuma 13 za Mkurugenzi Ileje kuchunguzwa