Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru akisubiri kusomewa shitaka linalomkabili.

Nassari amesema jana alikwenda kituo cha polisi Usa River kufuatilia silaha yake iliyochukuliwa na askari wakati wa uchunguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014.

Nassari amesema alipofika polisi alielezwa kuwa ana kesi ya kumshambulia mtendaji kosa analodaiwa kutenda mwaka 2014.

Sheki Mfinanga ambaye ni wakili wa Nassari amesema hajui mteja wake anakabiliwa na shtaka gani.

”Jana walisema alishambuliwa lakini hatujui leo anashitakiwa kwa kosa gani ndiyo tunasubiri,” amesema

Aliyesimamia kuapishwa kwa Raila ashtakiwa kwa uhaini
Daktari asakwa kwa kuambukiza VVU watu 21