Wanamuziki ambao pia ni wapenzi maarufu, Nareel na Aika wamepanga kufunga ndoa ya aina yake ‘punde si punde’.

Wanafamilia hao wa Navy Kenzo ambao wana mtoto mmoja aitwaye ‘Gold’ wamezungumzia ndoa yao ambapo Nareel amedai haitakuwa ya kawaida bali ndoa maalum.

“Sisi kwetu ndoa ni kitu special (maalum), kwahiyo na mimi nataka niifanye special (maalum) kwa Aika. Na unajua ukifanya kitu special ni lazima ujipange,” alisema.

“Ni maisha, kwahiyo ndoa inakuja, mimi na Aika ni very soon (hivi punde). Kwahiyo ndoa inakuja, mimi na Aika tunaitaka na tunataka iwe ni kitu ambacho tutaacha historia kwa ajili yetu na kwa watu wanaotupenda,” aliongeza.

Kwa upande wa Aika, alieleza kwa utani kuwa kwakuwa swali hilo kuhusu ndoa limeulizwa sana ndani ya kipindi cha wiki mbili, basi watatengeneza bango dogo na kuliandika ‘Ndoa Coming Very Soon’.

“Nareel ana bahati kukutana na msichana kama mimi ambaye sipendi vitu-vitu vya ndoa, napenda maisha yetu jinsi yalivyo. Ndoa itakuwa sehemu ya kitu kwenye maisha yetu lakini kwa jinsi tunavyoishi hivi sasa tayari uhusiano wetu ni imara, ni kama ndoa tayari,” alisema Mama Gold.

Wawili hao ambao uhusiano wao wa mapenzi una zaidi ya miaka 10, tangu wakiwa chuoni na baadaye kufanya muziki kama kundi la Navy Kenzo wameendelea kufanya vizuri nyumbani na hata kwenye anga za kimataifa.

Hivi karibuni waliachia audio na video ya wimbo wao mpya ‘Fella’.

Sekretarieti ya Maadili yawaweka mtegoni Wabunge
Peter Schmeichel amtetea Ben Youssef wa Tunisia