Mzunguko wa 22 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaendelea wikiendi hii Machi 11, 2018 kwa kuchezwa mechi tano (5)

Mechi mbili za mzunguko huo zilizokuwa zichezwe Machi 11, 2018 zimebadilishiwa tarehe.

Simba waliokuwa wacheze ugenini dhidi ya Njombe Mji mchezo huo sasa utapangiwa tarehe nyingine baada ya Simba kuomba kusogezwa kwa mchezo huo ili kupata muda wa maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry utakaochezwa Port Said nchini Misri Machi 17, 2018.

Mchezo wa Kagera na Mwadui uliokuwa uchezwe Machi 11, 2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba sasa utachezwa Jumanne Machi 13, 2018 kutokana na kusogezwa kwa mchezo wao dhidi ya Young Africans unaochezwa leo Machi 9, 2018.

Mechi nyingine za mzunguko wa 22 zitakazochezwa Jumapili Machi 11, 2018

AzamFC  vs Mbao FC (Azam Complex,Chamazi)

Ruvu Shooting vs Mbeya City  (Mabatini) 

Singida United vs Ndanda  (Namfua)

Majimaji vs Lipuli  (Majimaji)

Tanzania Prisons vs Mtibwa Sugar (Sokoine)

Video: Lissu ataja sababu za kutompuuza Musiba.
Simba Vs Al Masry waingiza milioni 85,045,000