Mahakama ya Eldoret nchini Kenya imemhukumu mzee wa kanisa kifungo cha maisha jela baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10.

Ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo ulieleza kuwa Starico Madegwa mwenye umri wa miaka 53 alifanya kosa hilo Machi 20, miaka mitatu iliyopita.

Wakati wa kusikiliza ushahidi, mtoto aliyedaiwa kutendewa unyama huo alieleza kuwa mshtakiwa aliwaambia watoto wake watoke nje na kisha akamtaka yeye abaki ndani na ndipo alipombaka.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Eldoret, Stella Telewa alieleza kuwa Mahakama imepata ushahidi wa kutosha katika kipindi chote cha kusikiliza kesi hiyo na umemtia hatiani mshtakiwa.

Baada ya kutangaza kifungo cha maisha jela, mahakama ilitoa siku 14 kwa mshtakiwa kukata rufaa.

Chris Brown aanza kupangua kesi ya nyani kukwepa jela
Serikali ya DRC yamtimua balozi wa Umoja wa Ulaya