Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ametaja sababu zilizomsukuma kutogombea tena ubunge kwa mwaka huu 2020 .

Mnyika ambaye kabla ya Bunge kuvunjwa alikuwa mbunge wa kibamba (2015 -2020) kupitia akaunti yake ya Twitter amesema huu ni wakati wake wa kupumzika ubunge na kujenga chama ili kipate ushindi kama Baba wa Taifa alivyokifanyia chama cha TANU.

“Nyerere aliwahi kuachia uwaziri Mkuu akabaki kuimarisha TANU, nami sitagombea ubunge 2020 nitumikie ipasavyo ukatibu mkuu CHADEMA, tushinde uchaguzi tulete mabadiliko” Amesema Mnyika.

Kada huyo aliyekaa Bungeni kwa vipindi viwili mfululizo (2010 -2020) amesema alifikia uamuzi huo kabla ya Disemba 2019 ambapo alichaguliwa kuwa katibu mkuu.

Jana jimbo la Kibamba katika kura za maoni za mgombea wa kupeperusha bendera ya ubunge kwa chama hicho alishinda Ernest Mgawe kwa kura 30 kati ya 71 za wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo.

Waliofuata nyuma yake ni Names Tarimo kwa kura 22, na Humphrey Sambo kwa kura 19.

Luc Eymael: Simba SC wametupa mwongozo
Prof. Kabudi: Sigombei kutafuta umaarufu