Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli, amemtangaza Dk. Hussein Ali Mwinyi amechaguliwa kwa kura 129 sawa na zaidi ya asilimia 78 za kura zote.

Dk. Mwinyi ambaye aliingia katika Tatu Bora na wagombea wengine Shamsi Vuia Nahodha aliyepata kura 16 sawa na asilimia zaidi ya tisa pamoja na Dkt. Khalid Salum Mohamed aliyepata kura 19 sawa na zaidi ya asilimia 11.

Baada ya kutangazwa mshindi, Dk Mwinyi amewashukuru wajumbe kwa kuwa na imani naye na kuahidi kuwa atalitumikia Taifa na kuomba kwa sasa kuwa na Timu ya Chama cha Mapinduzi kwa maendeleo ya Taifa.

Wakati huo huo aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM Abdurrahman Kinana amefutiwa adhabu yake ya miezi 18.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Dkt. John Magufuli ametangaza kumfutia adhabu ya miezi 18 aliyokuwa anaitumikia ambapo mpaka sasa ameshatumikia adhabu yake hiyo kwa miezi minne.

Magufuli ametangaza kuifuta adhabu hiyo wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, mjini Dodoma.

Bernard Morrison apaza sauti kwa mashabiki
Simba SC wafunguka usajili wa Morrison

Comments

comments