Aliyekuwa Diwani wa kata ya Mambwenkoswe kupitia tiketi ya Chadema  Kanowalia Julius Siwale kwa hiari yake ameamua kujiuzulu nafasi hiyo na kujivua uanachama wa Chadema kwa kile alichodai kuwa Chama hicho kimekuwa na migogoro isiyoleta tija na maendeleo katika jamii.

Hivyo rasmi kajiunga na CCM ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Joseph Pombe Magufuli.

Aidha jana katika mkutano wa kamati kuu ya CCM ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais John Pombe Magufuli alisema uamuzi unaofanywa na wanachama wa vyama vya upinzani ni uamuzi wa kishujaa na chama hicho kina wakaribisha ili kuungana katika kuwaletea wanachi maendeleo.

 

Fanyeni kazi acheni 'Kiki'- Jafo
Steven NZonzi kucheza Italia hadi 2022

Comments

comments