Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kuwa anatarajia kufanyiwa upasuaji wa mwisho ambao utakuwa upasuaji wa 23, ikiwa ni kumalizia hatua za mwisho za matibabu yake.

Amesema kuwa upasuaji huo atafanyiwa Februari 20, 2019 operesheni hiyo ya mwisho itafanyika kwenye mguu wake wa kulia ambao mpaka Desemba 31 ulikuwa umepasualiwa mara 10, huku tumboni akiwa amefanyiwa operesheni 5.

“Mwili wangu umechanwachanwa sio vya kuelezeka maana huu mguu wangu ulipigwa risasi 4, na mkono wangu sasa hivi haunyooki vizuri. na kuna risasi 7 zilitolewa tumboni.”amesema Lissu

Aidha, ameongeza kuwa mguu wake peke yake umefanyiwa operesheni 10 na 11 utafanyiwa Februari 20, kwa hiyo akivua suruali watu wanaweza kumkimbia kwasababu ya makovu aliyo nayo,

Mbunge huyo wa Singida Mashariki kwa sasa anafanya ziara nchi za nje baada ya kupata nafuu alipokuwa amelazwa nchini Ubelgiji.

Mwanaharakati aliyetoweka akutwa amefariki dunia
Mwigulu Nchemba apata ajali

Comments

comments