Mtoto anayekadiliwa kuwa na umri wa miezi 7 amekutwa ameuawa kikatili na mwili wake kutelekezwa katika kontena la taka lililopo soko la Kihesa Manispaa ya Iringa.

Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa mtaa wa sokoni Agustino Kimulike amesema kuwa dampo hilo linatumika na mitaa  mitatu hivyo kama serikali wanaendelea kushirikiana na wananchi ili kumbaini mwanamke aliyefanya kitendo  hicho.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Kihesa Swebe Datus amesema kuwa wananchi wanapaswa kukomesha matukio kama hayo kwani yanaleta sifa mbaya katika jamii.

Nao baadhi ya wananchi wa mtaa huo Kata ya Kihesa wamelaani wanawake na mabinti wanaofanya vitendo hivyo kuongeza kuwa kama hawana uwezo wa kulea ni vyema wakatumia uzazi wa mpango ili kuepuka kubeba mimba zisizotarajiwa.

Mwili wa mtoto huyo umechukuliwa na jeshi la polisi  kwa ajili ya taratibu za mazishi na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa lengo la kubaini mtu aliyefanya tukio hilo.

Video: Shepu bandia zenye gharama kubwa zaidi duniani, wasanii, watangazaji hawa watia fora
Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma Februari 6, 2019