Mbunge wa Iramba Magharibi kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Dkt. Mwigulu Nchemba amependekeza kuwa mtindo wa mavazi ambao yeye amekuwa akiuvaa mara kwa mara utumike kama vazi la taifa kwa kile alichokieleza umekuwa ukiwatambulisha Watanzania hasa wanapokuwa nje ya nchi.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo juu ya vazi rasmi la taifa.

Amesema kuwa Watanzania wakienda nje ya nchi huwa wanatumia skafu, tai yenye rangi ya bendera ya taifa kama kitambulisho cha taifa na hutambulika kwa haraka zaidi.

“Watanzania wakienda nje ya nchi wanatumia skafu, tai bendera ya taifa yani Mwigulu style na wanatambuliwa ni Watanzania, kwanini Serikali isiseme hili ndilo vazi la taifa?, alihoji Mwigulu

Akijibu swali hiyo, Naibu Waziri Juliana Shonza amesema kuwa kwasasa mchakato wa kulipata vazi la taifa ulishaanza upya hivyo watahakikisha wanapokea maoni ya watu mbalimbali.

 

Wema Sepetu aswekwa mahabusu
Polepole aonya, 'Hatutasita kuchukua hatua kali'