Mtu mmoja aliyeshiriki uvamizi katika benki ya CRDB tawi la Igoma jijini Mwanza, amefariki kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa kutekeleza tukio hilo.

Mtu huyo akiwa na wenzake walivamia benki Usiku na kukata bati la paa na dari ili kupata upenyo wa kuingia ndani kwa lengo la kutaka kuiba fedha.

Kamanda wa Polisi, ACP Muliro Jumanne amesema kundi hilo la majambazi bado idadi yao haijafahamika lakini walivamia na kuvunja eneo la nyuma la Benki hiyo.

Imeelezwa kuwa majambazi hao walifanikiwa kuvuruga droo za ofisi hizo lakini hawakuweza kufanikiwa kuiba fedha zilizokuwa zimehifadhiwa sehemu maalumu.

Tshishimbi awasihi Mashabiki/Wanachama
Simba Queens uso kwa macho na JKT Queens