Mwanamuziki maarufu na mkongwe Afrika, raia wa Cameroon, Manu Dibango amefariki dunia jana baada ya kupata maambukizi ya virusi vipya vya corona (Covid-19).

Dibango ambaye alipata umaarufu zaidi kwa kupiga saxophone, amefariki akiwa na umri wa miaka 86.

Anakumbukwa zaidi kwa jinsi alivyoweza kuweka pamoja vionjo vya asili, jazz na muziki wa funk. Aliifikia dunia zaidi kupitia wimbo wake Soul Makosa wa mwaka 1972.

Alifanya nyimbo kadhaa na watu maarufu kama mkali wa piano kutoka Marekani, Herbie Hancock na Fela Kuti wa Nigeria.

Mwaka 2009, mwanamuzki huyo alifungua kesi dhidi ya Michael Jackson akidai kuwa amemuibia vionjo vya wimbo wake ‘Soul Makossa’ na kuviweka kwenye nyimbo mbili za albam yake iliyoweka rekodi kubwa ya mauzo duniani, ‘Thriller’. Michael Jackson aliyamaliza nje ya mahakama.

 

Maalim Seif: Nasikia Chadema hawakumtendea vyema Lowassa, ana sababu
Mbowe athibitisha mwanaye kuugua corona, aeleza hali yake na alivyoupata