Evelyn Namukhula, mwanamke aliyejifungua watoto watano mwezi uliopita amefariki dunia Jumapili, akiwa hospitalini jijini Nairobi alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28, mkaazi wa kijiji cha Sosokhe, Kaunti ya Kakamega alianza kulalamika kuwa anasumbuliwa na kifua  siku ya Jumamosi, Aprili 7 na alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Moi ambako alilazwa pamoja na watoto wake watano.

Namukhula alizua gumzo baada ya kujifungua watoto wa kike watatu na wa kiume wawili kwa wakati mmoja, ambapo madaktari walimfanyia upasuaji uliofanikiwa, Machi 13 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Kakamega.

Lakini baadaye alihamishiwa katika hospitali ya MTRH iliyoko Eldoret baada ya afya ya mtoto mmoja kutokuwa nzuri.

Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya MTRH, Dkt. Wilson Arwasa aliimbia Citizen ya Kenya kuwa magari ya wagonjwa (ambulance) matano yalitumika kuwasafirisha watoto wa mwanamke huyo wakiwa katika magari tofauti. Alisema joto lao lilikuwa bado liko chini sana walipofika hospitalini hapo, lakini baadaye walipata joto la kawaida.

Marehemu pamoja na mumewe, Herbert Wawire tayari walikuwa na watoto wanne ambao waliishi nao katika kijiji cha Sisokhe.

Bonta afafanua kilio chake kwa DC Jokate kuhusu wimbo wa ‘Tokomeza Zero’
Abiria wamchapa dereva kwa uendeshaji mbaya