Mwanamke mmoja Nchini Msumbiji amejifungua mtoto juu ya mti wa mwembe alipokuwa akiyakwepa maji yaliosababishwa na kimbunga Idai.

Mama huyo aliyefahamika kwa jina la Amelia amejifungua mtoto wa kike Sara alipokuwa juu ya mti na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka miwili.

Kwa mujibu wa BBC familia yao iliweza kuokolewa siku mbili baadaye na majirani kufuatiwa na dhoruba ambalo limeua watu takribani 700 nchini humo.

Hata hivyo Amelia ameliambia shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF kuwa “Nilikuwa nyumbani na mwanangu wa kiume mwenye umri wa miaka miwili ambapo ghafla , bila onyo lolote, maji yalianza kuingia ndani ya nyumba yetu,”.

“Sikuwa na njia nyingine ila kukwea mti, nilikuwa peke yangu na mtoto wangu wa kiume.”amesema Amelia.

Kwasasa Amelia na familia yake wanaishi katika makazi ya muda ya msaada karibu na Dombe, na wanaarifiwa kuwa katika afya nzuri.

Takribani miongo miwili imepita tokea tukio kama hilo kutokea, ambapo mtoto alizaliwa katika mazingira kama hayo aliejulikana kwa jina la Rosita Mabuiango, alizaliwa wakati wa mafuriko yalipokumba maeneo ya kusini mwa Msumbiji.

 

Lema azungumza baada ya kuadhibiwa bungeni, awapa ujumbe wabunge
JPM amfagilia Mkapa, 'Bila yeye nisingekuwa waziri au Rais'