Mwanamke  Lilly Ajarova, kutoka nchini Uganda, amejitolea kuwa mama wa sokwe yatima ambao huokolewa na kupelekwa katika hifadhi anayofanya kazi ambayo kwasasa amekuwa mkurugenzi mkuu wa hifadhi hiyo.

Hifadhi hiyo ya Ngamba sanctuary, ipo karibu na ziwa Victoria ambayo hukusanya nyani aina ya sokwe kutoka katika ukanda wa Afrika mashariki na kuwatunza.

Lilly ambaye wengi humuita mama sokwe, amekuwa akifanya kazi ya kuwahifadhi kwa miaka 13, kwa kuhakikisha  nyani wote walio okolewa wanakuwa salama na kuwaondoa hofu ya kuuwawa na wawindaji.

Kwakutambua jinsi anavyowajali wanyama kwa kuwalea vizuri,kuwapa malisho na usalama, amechaguliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa bodi ya utalii ya Uganda (UTB)

 

Wazee 25499 kutibiwa bure wilayani Magu
TFDA yajivunia mafanikio ndani ya miaka 3 ya JPM

Comments

comments