Katika hali ya kustaajabisha,Grolia Arnord (33) mkazi wa njia panda wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro ameishi na minyororo kwa muda wa miaka mitatu, kwa kuwa ana matatizo ya akili.

Imeelezwa kuwa  amefungwa minyororo kumuepusha kutoroka nyumbani kwenda mitaani ambapo amekuwa akifanyiwa vitendo vya udhalilishaji ikiwemo kubakwa na kuambukizwa virusi vya ukimwi.

Mama mazazi wa mtoto huyo Vaileth Tarimo (67) amesema kuwa alimzaa Grolia mwaka 1987 akiwa mzima na akili timamu.

”Mtoto wangu nilijifungua akiwa salama lakini alipofikisha umri wa miezi sita nikiwa nimetoka kazini kuja kumnyonyesha ndipo jirani alipokuja na kumwagia chumvi mwanangu wakati namnyonyesha” amesema Vaileth

Kwa mujibu wa gazeti a Uhuru mara baada ya tukio hilo aliamua kuchukua uamuizi wakwenda Polisi kumfungulia kesi ambapo ndugu zake walimsihi kesi hiyo izungumzwe na wasameheane.

Mama huyo ameongeza kuwa Gloria hakutambaa tena wala kusema chochote mpaka alipofikia umri wamwaka mmoja na miezi minne baada ya kuangaika ndipo akaanza kutembea.

Vaileth ameeleza mtoto wake alishindwa kuendelea na masomo baada ya kuanza kutoroka nyumbani akiwa darasa la pili na kwenda kusiko julikana.

Amebainisha kuwa mwaka 2006 alitoroka nyumbani na kurubuniwa na wanaume ambao walimnywesha pombe na hatimaye alibeba ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume ambaye kwa sasa yupo darasa la sita katika shule ya msingi Dk SHein.

”Mara nyingi amekuwa akitoroka nyakati za usiku nimekuwa nikiteseka mwenyewe kumtafuta hali ambayo imenisbabishia kupata ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu” alisema

Hata hivyo amesema aliamua kufanya uamuzi wa kumfungia ndani kwa minyororo mwaka 2016 ili kuhakikisha kuwa hatoroki nyumbani lakini aliona suala hilo ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mama huyo amesema kuwa aliamua kutumia njia hiyo akiona ndio njia sahihi ya kuhakikisha  Gloria atabaki nyumbani lakini amekuwa bado akitoroka, kitu amabcho kimepelekea kuambukizwa virusi vya ukimwi.

Aidha Vaileth ameiomba serikali imsaidie ili mwanaume aliyemharibia maisha mtoto wake achukuliwe hatua za kisheria kwani anamjua aliyefanya hivyo lakini hajui wapi atapata haki ya mtoto wake.

Kilwa: DC akemea wananchi waliowaita wazungu Corona
Afariki ajalini akiiba pikipiki