Mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la wananchi (JWTZ) aliyestaafu akiwa na cheo cha meja mwenye umri wa miaka 54, anashikiliwa na polisi mkoani katavi kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi watatu kwa nyakati tofauti.

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga ametoa taarifa ya tukio hilo kwa waandishi wa habari jana, na kusema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa na anaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

Amesema katika tukio la kwanza na la pili mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo kwa wanafunzi wa familia moja kwa nyakati tofauti dada na mdogowake wenye umri wa miaka 13 na 14 na kuwapa fedha Tsh. 20, 000 kila mmoja.

Katika tukio jingine mtuhumiwa huyo anadaiwa mnamo Machi mosi mwaka huu katika mtaa wa Tambukareli kwenye nyumba ya kulala wageni majira ya saa tatu usiku alimbaka mwanafunzi wa darasa la tatu majira ya saa tatu usiku na kumahidi kumpa zawadi ambazo hakumpa.

” Ilipofika majira ya saa 4 usiku alirudi myumbani kwao na kumkuta mama yake aitwaye Frola Pascal ambaye alimuuliza alipokuwa na akamwambia hali halisi”

“Kisha mama wa mtoto huyo alimtaka mwanaye ampatie nguo alizokuwa amevaa kwaajili ya kuzikagua kisaha aliamua kwenda kituo cha polisi Mpanda kwaajili ya kutoa taarifa za tukio hilo” amefafanua kamanda huyo.

Hata hivyo kamanda kuzaga amesema kuwa upelelezi utakapo kamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

India: Wabakaji wa mwanafunzi kwenye basi wanyongwa
Video: Wagonjwa wa Corona waongezeka Tanzania, Membe akoleza moto wa tume huru