Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Kigoma imemuachia huru Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Nyantore wilayani Kigoma baada ya upande wa mashtaka kuomba kutoendelea na shauri hilo kufuatia shahidi wa pili mwanafunzi mwenye mimba kueleza mbele ya mahakama kuwa hamfahamu mtu aliyeshiriki naye mapenzi hadi kupata mimba.

Lakini pia shahidi huyo amekana kuwa na umri wa miaka 16 kama upande wa mashtaka ulivyoeleza awali kupitia upelelezi wa polisi.

Naye baba wa mwanafunzi huyo amesema kuwa binti yake ana umri wa miaka 19 na kwamba polisi walikuwa wakimshawishi aseme ana umri wa miaka 16 tofauti na anavyofahamu.

Kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilisomwa Agosti 14, 2019 ambapo shahidi wa kwanza mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Sakina Kazili (55) aliiambia mahakama Septemba 12 binti yake ana umri wa miaka 16 na kwamba alizaliwa februari 7, 2003.

Hakimu mfawidhi wa mahakama, Flora Mtarania amesema anakubali ombi la upande wa mashtaka kufuta shauri hilo na kwamba uamuzi huo hauzuii kumkamata tena mtuhumiwa huyo, Jason Rwekaza endapo atabainika kuwepo sababu za kufanya hivyo.

 

Rais Magufuli apiga marufuku tozo machinjio ya Vingunguti
Askofu mkuu Dar es salaam, Ruwa’ichi atolewa ICU