Mtahiniwa wa mtihani wa taifa kidato cha nne katika shule ya upili ya wasichana ya Ngata kaunti ya Nakuru amekataa kufanya mtihani kwa madai kuwa hakuwa amejiandaa vilivivyo.

Mwanafunzi huyo aliwaelezea wasimamizi wa mtihani huo kwamba alijifungua mtoto wake wa kwanza miezi mitatu iliyopita na hajakuwa na wakati wa kujisomea mtihani.

kithibitisha kisa hicho, naibu kamshna wa kaunti ya Nakuru, Julius Kavita aliwaambia wanahabari wa K24 kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ashawasiliana na wakuu wa elimu kuhusiana na uamuzi wake.

Juhudi za kumshawishi mwanafunzi huyo huufanya mtihani hazikufaulu huku akisisitiza kuwa atajisajili upya kwa mtihani huo mwaka wa 2020.

Mtihani wa kitaifa, KCSE ulianza rasmi Jumanne, Novemba 4, huku watahiniwa 699,745 wakitarajiwa kuufanya mtihani huo.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 6, 2019
Agizo la Jafo kwa wagombewa walioonewa

Comments

comments