Mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Fatuma Makaranga (15), amefariki dunia kwa madai ya kujitumbukiza ndani ya tangi la maji baada ya kutokea mtafaruku baina yake na familia yake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Murilo Jumanne amesema Juni 4, mwaka huu majira ya saa 5 usiku katika mtaa wa Ndofe wilayani Nyamagana walipata taarifa ya kifo hicho.

“Alikutwa akiwa amefariki na mwili wake ukiwa ndani ya tangi la maji lililopo nyumbani kwao baada ya harufu mbaya iliyokuwa ikitokea ndani ya tangi hilo” Amesema Murilo.

Amesema kifo hicho kimetokana na mtafaruku mkubwa uliotokea baina yake na baba yake mzazi, ndipo mwanafunzi huyo akuamua kuondoka kwao kuelekea kusikojulikana.

“Baada ya wazazi wake kumtafuata bila mafanikio, walitoa taarifa katika kituo cha polisi Nyakato na baada ya siku kadhaa kupita walianza kusikia harufu mbaya ikitokea ndani ya tangi hilo” Ameeleza KAmanda Murilo.

Na kuongeza kuwa ” Ndipo baba alipoamuru wamwage maji walifanyie usafi, shughuli ya kusafisha ilipoanza ndipo walipokuta mwili wa binti huyo”.

Aidha amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kufanyika ili kubanini zaidi chanzo cha kifo hicho.

Tetesi za usajili barani Ulaya
Lille Olympique: Arsenal wajiandae

Comments

comments