Mkali wa michano na misemo, Hamisi ‘Mwana FA’ Mwinjuma pamoja na muigizaji wa filamu za Kiswahili, Single Mtambalike wamechaguliwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Wasanii hao wameteuliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakiwa kati ya wajumbe watano wa Bodi ya wakurugenzi ya baraza hilo.

Uteuzi huo umefanyika baada ya Rais John Magufuli kumteua Habbi Gunze kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo mpya.

Wengine walioteuliwa pamojana wasanii hao ni Bi. Asha Mshana ambaye ni Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Sanaa na Utamaduni ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Dkt. Emmanuel Ishengoma ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma; pamoja na Dkt. Saudin Mwakaje ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Uteuzi wa Mwana FA na Richie umepokelewa kwa mtazamo chanya na wadau wa sanaa nchini ambao wanaona wamepata uwakilishi mzuri kwenye bodi hiyo.

Richie

Mbali na ukubwa wa kazi zake, Mwana FA amewahi kuwa sehemu ya uongozi wa chama cha wasanii nchini na msomi mwenye shahada ya uzamili.

Richie ni mmoja kati ya waigizaji maarufu zaidi nchini wenye alama ya kazi nzuri.

Dar24 inawapongeza na kuwatakia kila la kheri wanapoanza kazi hiyo muhimu

Kubenea adai Meya Boniface ndiye ‘wa karibu zaidi’
Waziri Mkuu aliyepiga ‘push up’ na wanajeshi adai walitaka kumuua