Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari  10, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;

Mchezo namba 190: Yanga SC 2 vs 1 Lipuli FC

Mwamuzi Abubakar Mturo amefungiwa miezi mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39(1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Vile vile katika mchezo huo mwamuzi msaidizi namba mbili Joseph Pombe amefungiwa miezi mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39(1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Mchezo namba 189: Azam FC 1 -1 Tanzania Prisons FC

Morris amepigwa faini ya kiasi cha Tsh 200,000/=(Laki Mbili) kwa kosa la kugoma kuongea na  waandishi wa habari  mara baada ya mchezo kumalizika katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Adhabu hii imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Bodi ya ligi yamuonya kocha Vandenbroeck
Rufaa ya Rais Mutharika yakataliwa

Comments

comments