Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limemkamata Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Zanzibar, Salum Mwalimu aliyekuwa mkoani humo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, Mwalimu amekamatwa na jeshi la polisi akiwa kwenye gari akitokea Kanda ya Nyasa.

Ameeleza kuwa kiongozi huyo mwandamizi wa Chadema alikamatwa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, leo Jumapili ya Disemba 16 alipokuwa anaingia mkoani humo kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya ndani vya chama.

Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar)

“Nimepata taarifa kuwa amekamatwa akiwa anaelekea katika vikao vya ndani vya chama hapo Mafinga. Alikuwa anatokea Kanda ya Nyasa, kama unavyojua tunaendelea na program ya ujenzi wa chama ikiwa ni pamoja na ile ya ‘Chadema ni Msingi’,” Makene anakaririwa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa hakupatikana kwa muda kuelezea taarifa hizo akieleza kuwa yuko kwenye kikao. Hivyo, bado sababu hasa za kukamatwa kwake hazijafahamika.

Njia 6 Rahisi za Kuwa Imara Wiki Yako ya Kwanza Kazini
Mabillioni yalipwa kwa wakulima wa Korosho