Mwalimu Focus Mbilinyi aliyekuwa akifundisha Shule ya Msingi Madeke amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela pamoja na kulipa fidia ya Tsh. Milioni 10 baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga Hosea Manga na kumsababishia ulemavu wa kudumu.

Focus Mbilinyi alimuadhibu mtoto huyo kwa mtindo wa kumning’iniza miguu juu ya dirisha huku kichwa kikiwa chini hali iliyompelekea kuanguka na kuvunjika kwa visahani vya uti wa mgongo.

Mahakama imemtia hatiani Focus kupitia kifungu cha Sheria namba 235 kifungu kidogo cha 1 cha Kanuni ya Adhabu namba 20 na kifungu cha Sheria namba 348 kifungu kidogo cha kwanza cha Kanuni ya Adhabu namba 20.

Mwalimu Mbilinyi alitenda kosa hilo Machi 21, 2017 kijiji cha Madeke.

India: Waandamanaji zaidi ya 10 wauawa
Nigeria: Gavana atangaza mapumziko siku ya kumpokea Rais

Comments

comments