Mwalimu wa shule ya sekondari ya Kibwe jijini Dodoma, Nocka Mwaisango (28), mkazi wa Mbalizi mkoani Mbeya , amefariki dunia kwa kunyweshwa sumu na watu wasiojulikana na kupelekea kupoteza maisha.

Kabla ya kufariki Mwaisambo alikuwa safarini kutoka mkoani Dodoma kuelekea jijini Mbeya kwaajili ya kumchumbia mchumba wake wa muda mrefu.

Baba wa marehemu Oddy Mwaisango, alipozungumza na waandishi wa habari ameeleza kuwa mtoto wake alimpigia simu kuwa yupo katika maandalizi ya kurudi nyumbani kwa mapumziko na atatumia nafasi hiyo kumchumbia mpenzi wake wa muda mrefu.

Mzazi huyo amesema hawakupata wasiwasi wowote hadi ilipopita wikimoja akapigiwa simu na watu ambao hawakujitambulisha na kwamwambia asiwe na hofu juu ya ukimya wa mwanae yupo salama, ndipo alipo amua kuanza kumtafuta.

“Baada ya simu hiyo nilienda polisi kutoa taarifa na siku iliyofuata mkewangu alienda mkoani Dodoma kufuatilia katika shule aliyokuwa anafundisha na mkuu wa shule alimjibu hana taarifa ya safari ya mwanae”

Uchunguzi wa polisi ulipoanza, walipokea simu ya marehemu aliyeeleza kuwa yupo kituo cha magari, Tazara jijini Mbeya na walipo mfuata walimkuta hajitambui hadi walipomkimbiza hospitali ya rufaa Mbeya.

Akiwa hospitali alilalamika koo linamuuma , baada ya Daktari kuchukua vipimo walibaini kuwa amenyweshwa sumu na juhudi za kumuokoa ziligonga mwamba.

Kamanda wa polisi jijini Dodoma Gilles Muroto, amesema kuwa amepokea taarifa za kifo cha mwalimu huyo lakini hatoweza kutoa taarifa kamili ya uchunguzi kwani yupo nje ya ofisi.

 

 

Simba yaanza kuitafuna JS Saoura ya Algeria taratibu
Mlipuko wa mafuta waua 12

Comments

comments