Mwalimu wa shule ya sekondari ya Matemanga iliyopo Ruvuma wilayani Tunduru, Hekima Gregory maarufu Mvomela (49), amefariki baada ya kunywa pombe aina ya gongo.

Kwamujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa amesema taarifa juu ya tukio hilo ilitolewa kwenye kituo cha polisi cha Matemanga kutoka kwa mratibu elimu kata ya Matemanga, Rashidi Nasoro.

Kamanda Marwa amesema katika taarifa hiyo, Nasoro alieleza kuwa mwalimu Gregory alikutwa akiwa amekunywa pombe ya kienyeji aina ya gongo na inadaiwa kuwa alikuwa hajapata chakula.

Ameeleza kuwa baada ya kumkuta mwalimu huyo akiwa amelewa ‘chakari’, hatua ya kwanza walimchukua na kumpeleka hospitali ya misheni ya Kiuma ambako alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu.

Taarifa hiyo imeeleza pia marehemu katika historia yake ilikuwa kawaida yake kunywa pombe kwa kupindukia bila kula chakula cha kutosha licha ya kuonywa mara kwa mara na viongozi wake.

Tayari jeshi la polisi linawashikilia watu watatu waliokutwa na lita 3.5 za pombe hiyo ya kienyeji.

R Kelly akabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela
Maelfu waandamana kupinga Serikali ya George Weah

Comments

comments