Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Habari,Utalii Utamaduni na Michezo ya Zanzibar zimekubaliana kushirikiana katika Michezo ikiwa ni mikakati ya kuleta mafanikio ya soka ndani na nje ya nchi hizo.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa lengo la kukutana na Waziri mwenye Dhamana ya Michezo visiwani Zanzibar ni kutimiza lengo la muda mrefu la kukutana na kupanga mikakati mbali mbali ya kuinua soka la nchi hizo.

“Tumekutana kuweka mikakati imara ya kutimiza lengo la muda mrefu la kutafuta njia mbalimbali zitakazosaidia soka letu kukua na kuimarika ndani na nje ya ya nchi zetu”,Amesema Dkt.Mwakyembe.

Aidha ameipongeza Zanzibar kwa kufanikiwa kuwa mwanachama halali wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika(CAF) na ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika maendeleo ya soka ya nchi hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Habari  Utalii Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Rashidi Waziri  amesema kuwa Wizara yake ina jukumu kubwa kuendeleza Soka la Zanzibar hasa katika kipindi hiki amabacho imepata nafasi katika Shirikisho la mpira wa miguu la Afrika.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ushirikiano wa Kisoka baina ya Wizara hizo utaleta hamasa kwa wawekezaji wa soka kupata uwanja mpana wa uwekezaji kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

 

Serikali kutatua kero ya maji Chalinze
Live: Maswali na Majibu Bungeni Dodoma