Mamlaka ya hali ya hewa(TMA) imesema utabiri wa hali ya hewa juu ya joto kali ambao waliutoa january 7 mwaka huu bado upo palepale.

Mkurugenzi wa utabiri (TMA) Samweli Mbuya amesema hali ya joto bado inaendelea na inazidi kuongezeka siku hadi siku na kubainisha kuwa, mvua zinazoendelea kunyesha baadhi ya maeneo nchini hazihusiani na kupungua kwa kiwango cha joto kwenye maeneo mengine.

Katika utabiri uliotolewa na TMA january 7 mwaka huu ulisema kiwango cha joto kwa baadhi ya maeneo ikiwemo mikoa ya Pwani, Tanga, Dar es Salaam na Zanzibar umefikia nyuzi joto 34 kiwango ambacho ni juu ya wastani.

Hata hivyo kiwango hicho kiliongezeka na kufikia nyuzi joto 35.4 katika baadhi ya maeneo ikiwemo kibaha mkoani Pwani na Zanzibar hali iliyoweka watu wengi roho juu kwakuwa haikuzoeleka.

” Maeneo ya Kibaha na Zanzibar joto lilikuwa nyuzi joto 35.4 pamoja na kuwepo mvua katika maeneo machache” amesema Mbuya.

Dkt. Andrew Foi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema mabadiliko yoyote ya hali ya hewa yana madhara katika maisha ya mwanadamu ambapo amesema joto linapozidi kila mtu anaathirika kutokana na maumbile au umri wake.

”Watoto wadogo katika kipindi cha joto wanatoka vipele sana hasa hawa ambao wapo chini ya umri wa miaka mitano, kwa upande wa watu wanenene wanaweza kupata muwasho na bakteria katika pakachu za mwili pia kuna watu wanatoka majipu sana katika kipindi cha joto. amesema Dkt Foi.

Aidha amesema joto linapozidi linaweza kusababisha mtu kupoteza fahamu ni vizuri kwa watu wanaofanya kazi katika sehemu zenye joto kali kuwa makini hasa kipindi hiki.

 

Tiketi za mabasi sasa kieletroniki
Mo atengua kauli, arudia nafasi yake baada ya kujiuzulu "Mimi ni simba damu"