Kamati Kuu ya Utendaji ya Chama Tawala Nchini Uganda, National Resistance Movement (NRM), imemuidhinisha rais wa sasa, Yoweri Museveni kugombea urais mwaka 2021 na katika chaguzi zote zitakazofuatia kwa mda wa miaka 50 ijayo.

Uamuzi huo umefikiwa wakati wa kufunga kikao maalum cha viongozi wakuu wa chama cha NRM kilichofanyika katika Wilaya ya Nwoya baada ya muswada uliowasilishwa na kukubaliwa na kamati nzima.

Kwa mujibu wa maamuzi ya kamati kuu ya chama hicho, viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho ambacho kimeitawala Uganda tangu mwaka 1986, wamemuidhinisha Museveni kuitawala Uganda maisha yake yote.

Aidha, Kamati Kuu ya NRM imesema kuwa uamuzi huo umezingatia rekodi ya kisiasa na kiuchumi ya Museveni mwenye umri wa miaka 74, ndani ya Uganda, juhudi za kidiplomasia na majirani wa Uganda, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla kabla ya kumuidhinisha, bila yeyote kati yao kupinga.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa za Uganda akiwemo, Nabende Wamoto, wametoa mtazamo kwamba upinzani wa Uganda umegawanyika, hauna umoja hivyo hauwezi kumshinda Museveni katika uchaguzi zijazo.

Trump aweka kisiki kwa mrembo wa IS aliyetaka kurejea Marekani
Akaunti ya Instagram ya marehemu Godzilla yaibiwa