Baada ya kuenea na  kuwepo kwa  Maandamano ya vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo na Vyama vya upinzani kudai kutaka kuandamana leo jijini Dodoma kutaka  kulishinikiza Bunge kufuta azimio lake la kutofanya kazi na mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Prof. Musa Assad Jeshi la  Polisi limeimarisha ulinzi kila kona ya Mji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto, Akizungumza na waandishi wahabari leo amesema kuwa Makao makuu ya Nchi ni lazima yalindwe kwa gharama yeyote ambapo Jeshi leo limeimarisha  ulinzi kila kona ya mji kutokana na tukio la Chama cha   ACT-Wazalendo pamoja na  Vyama vya Upinzani kutaka kuandamana.

Kutokana na hali hiyo Kamanda Muroto amesema kuwa Mkoa wa Dodoma ni Makao makuu ya nchi hivyo jeshi la Polisi halitakuwa tayari kumvumilia mtu yeyote atakayetaka kuvuruga amani kwa kisingizio chochote kile.

“Kama mnakumbuka jana wakati naongea nanyi ndugu waandishi wa habari  kuwa watapigwa hadi wachakae tulikuwa hatutanii hivyo kama wangeweza kuingia barabarani kuandamana leo wangeona kipigo chao”amesisitiza Muroto.

Muroto amesema kuwa Jeshi la Polisi tangu leo asubuhi limeibarisha  ulinzi kila kona ya mji kwa  kutumia akari wa vikosi vya Mbwa na Farasi,Askari kanzu pamoja na kikosi cha FUU kwa kuzunguka maeneo ya mji.

“Nashukuru Mungu mpaka muda huu hakuna aliyeingia mtaani kuandamana ,nadhani wametii wangejaribu wangekumbana na kipigo na wangechakaa bila huruma kwa njia yoyote wasingepona ”amesema Muroto.

Ulinzi huo umeimarishwa  kutokana na chama cha ACT- Wazalendo pamoja na Vyama vingine vya upinzani vya NCCR Mageuzi,Chauma na UPDP  kutaka kuandamana kwenda Bungeni kushinikiza kufanyakazi na CAG Prof Musa Assad.

LIVE: Waziri Mkuu akihutubia Bungeni Dodoma muda huu
Je unatafuta ajira?, Hizi hapa nafasi 10 za ajira kwa ajili yako