Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ametoa onyo kali kwa watu wenye tabia za ubakaji na udhalilishaji wa kingono kwa watoto na wanawake, na kusema kwamba kwenye wilaya yake iwapo mtu atakamatwa hatopewa dhamana.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na umati uliokuwa ukimsikiliza wilayani humo kwamba mtu yeyote atakayekamatwa kwa makosa ya ubakaji na udhalilishaji wa kingono, ajue wazi kuwa hatopata dhamana akiwa kituoni, labda iwe mbele ya mahakama.

“Watu wenye vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watoto, wanawake na kina mama, katika Wilaya yetu huna dhamana, utakapopelekwa kituo cha polisi, tunajua dhamana ni haki yako, lakini katika hili Arumeru tumejiwekea utaratibu, hautapata dhamana, utashikiliwa mpaka kesi itakapokwisha, polisi huku tutakushikilia, hautapewa dhamana kituo cha polisi, omba Mungu ukapewe dhamana mahakamani kama utapelekwa mahakamani ukapewa dhamana mahakamani”, amesema Jerry Muro

Aidha, amesema kuwa iwapo atalalamikiwa kukiuka kwa haki za binadamu kwa kumnyima dhamana mbakaji, ni vyema wakajiuliza iwapo haki hizo zinaruhusu kufanya maovu hayo, na iwapo hairuhusu basi wajue wazi kuwa hata wao hakili yao ya dhamana haitapatikana.

Jerry Muro pia amewasisitiza vijana waendesha boda boda wa ndani ya mkoa huo kujiepusha na vitendo hivyo, kwani wamekuwa wakisifika kwa kufanya maovu kumalizia ‘handasi’ zao kama alivyoitaja.

Video: Masauni amvaa Katibu mkuu, ' Huyu hatufai kabisa'
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 22, 2019