Mwanaharakati na mcheza filamu, Whoopi Goldberg aliyecheza filamu maarufu ya Sarafina amezindua bidhaa yenye bangi maalumu kwa kupooza maumivu ya tumbo kwa mwanamke wakati wa hedhi.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 60, mfanyabiashara, mchekeshaji na mtangazaji wa vipindi katika televisheni za New York ambaye amekuwa akipigania juu ya matumizi sahihi ya bangi amesema bidhaa hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa mwezi ujao.

Ameongezea kuwa bidhaa hiyo si kwa ajili ya kulewesha bali maalumu kwa kupooza maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi na kumfanya mtu ajisikie huru.

Hivyo amekuja na njia hiyo mbadala kwa lengo la kuwasaidia wanawake wanaopata maumivu makali wakati wa siku zao za hedhi.

Ambapo bidhaa hiyo inatarajiwa kupatikana mji wa Califonia.

Ameongezea kuwa bidhaa hiyo inaweza pia kutumika kama kiungo cha chai.

Video: Ripoti ya CAG madudu kila kona, Mauaji ya watoto yametia doa Njombe - Magufuli
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 11, 2019

Comments

comments