Muigizaji mkongwe wa nchini Misri, Ragaa El-Gedawy amefariki baada ya kupata maambukizi ya virusi vipya vya corona (covid-19).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la Misri, muigizaji huyo amefariki leo, Julai 5, 2020 akiwa na umri wa miaka 81.

“Ragaa al-Geddawy amefariki leo asubuhi kwa covid-19, hatutafanya mazishi yanayoshirikisha umma kutokana na sababu za kiafya,” Mkuu wa Umoja wa Waigizaji wa Misri, Ashraf Zaki ameliambia Shirika la Habari la AFP.

Gedawy alibainika kuwa na virusi vya corona tangu Mei, 2020 na alikuwa akipatiwa matibabu katika eneo maalum lililotengwa katika Hospitali ya Ismailia, Kilometa chache kutoka jiji la Cairo.

Muigizaji huyo mkongwe amepata umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kuigiza tangu akiwa msichana. Hivi karibuni, alikuwa amekamilisha tamthilia ya Laabet El Nesyan (Oblivion Game) iliyorushwa kwenye vituo vya runinga wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadan.

Misri imethibitisha kuwa na visa 74,035 vya corona, wagonjwa 20,103 na vifo 3,280.

Tshishimbi, Morrison wakatwa safari ya Mara, Kagera

FBI wanavyomnyoosha ‘Hushpuppi’, mwizi nguli mtandaoni

Kanye West atangaza nia kumng’oa Trump kwenye Urais 2020
IGP Sirro ahimiza usajili kampuni binafsi za ulinzi kwenye PSGP, aeleza faida