Muigizaji maarufu, Idris Elba ametangaza kuwa amepima na kukutwa na virusi vya corona na kwamba alijitenga kwenye ‘karantini’ kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa watu wengine.

Akizungumza kwenye video fupi aliyoiweka kwenye akaunti yake ya Twitter muda mfupi uliopita, ikiambatana na ujumbe wa maandishi, Idris amesema kuwa alikutana na mtu mmoja ambaye baadaye aliugua na kukutwa na virusi vya corona, hivyo akachukua hatua ya kupima.

“Niligundua Ijumaa kuwa walikutwa na virusi vya corona, nikachukua hatua haraka na kufanyiwa vipimo, nikajitenga binafsi kwenye karantini. Na leo nimepata matokeo ya vipimo kuwa nina virusi vya corona,” alisema.

Katika ujumbe wake wa maandishi alieleza kuwa baada ya kupatiwa matibabu hivi sasa anaendelea vizuri na hana dalili zozote za virusi hivyo tena. Aliwaasa watu kubaki majumbani. Aliahidi kuendelea kutoa taarifa kuhusu hali yake.

Uingereza ni moja kati ya nchi za Ulaya zilizorekodi kesi za wagonjwa wa virusi vya corona. Serikali ya nchi hiyo imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuahirisha matukio yote ya michezo.

Video: Kikongwe afa kwa kubakwa akienda kanisani, Korona yauwa 6,500
Diamond ashtakiwa Mahakamani, akabiliwa na mashtaka mawili

Comments

comments